Kamati ya siasa ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya CDE Silvester M. Lwila wamefanya ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya maendele katika Halmashsuri ya Wilaya ya Momba kwa kutembelea miradi ifuatayo
1. Ujenzi wa soko la kimkakati la Mazao ya Kilimo na Mifugo (jengo la ghala, Mnada wa Mifugo na Soko la Mazao)- Kakozi
2. Shule ya sekondari Chitete (vyumba viwili vya madarasa)
3. ujenzi wa nyumba mkurugenzi
4. Jengo la utawala na
5. KItuo cha Afya Mkulwe
Kamati ilifurahishwa sana na namna utekelezaji wa miradi ulivyo shika kasi na kutekelezwa kwa wakati
aidha Mwenyekiti wa kamati ya siasa alitoa ushauri kwa watumishi kuzidi na kuongeza hali katika kumsaidia mkurugenzi kutimiza majukumu kwa kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na kusaidia miradi kukamilika kwa wakati na kusaidia wananchi wapate huduma kwa haraka kama Serikali ilivyo kusudia.
Pia kamati ilitoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba Mhe. Mathew Chikoti kwa usimamizi wake Madhubuti wa miradi ya maendeleo
"Hakika mnatendea haki miradi na imani ya Mh. Raisi kwa kuamua kuielekeza miradi hii ya Maendeleo kuletwa Halmashauri ya Momba , Nizidi kuwasihi endeeni na kasi na ikibidi kumaliza mapema zaidi ya muda uliopangwa iliwengine nao wajifunge kupitia sisi."
Tunduma-Momba
Postal Address: S.L.P 273 Tunduma Momba
Telephone: 0252957476
Mobile: 025 295 7476
Email: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc