WAFUNDISHENI VIJANA KUUNDA VIKUNDI WAKOPESHWE ASILIMIA 10% ZA SERIKALI.
Ikiwa ni Mwendelezo wa Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. KENANI KIHONGOSI katika kata ya Ivuna na Nzoka Tarehe 23/04/2024 amewaelekeza Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Halmashauri mpka ngazi ya Kata kuwafundisha vijana namna bora ya kuunda vikundi ili waweze kupata mkopo wa Asilimia 10% kutoka Serikalini.
Aidha, Amewasihi sana Vijana kuwa wazalendo kwa nchi yao na kuacha kushinda kwenye michezo na makundi mabaya na wajikite zaidi kwenye fursa mbalimbali kama vile Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Tunduma-Momba
Postal Address: S.L.P 273 Tunduma Momba
Telephone: 0252957476
Mobile: 025 295 7476
Email: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc