WAGANGA WA TIBA ASILI MOMBA WAKABIDHIWA VYETI VYA USAJILI WA MUDA
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba Ndg. Alex Batweli akabidhi vyeti vya usajili wa muda kwa Waganga wa tiba Asili ambapo katika makabidhiano hayo Batweli amesema:-
Lengo la serikali ni kuhakikisha waganga wote wa Tiba Asili wanapata usajili wa kuendesha shughuli zao kwa kufuata taratibu na miongozo ya Wizara ya Afya.
Pia waganga wa Tiba Asili wajisali ili watambulike na waweze kutoa taarifa zao za kitabibu kwenye mamlaka na mifumo ya serikali ya kutolea huduma za afya.
Waganga wa tiba asili wanawajibu wa kutoa taarifa zao za kitabibu na pia kutoa rufaa ya wagonjwa wanaofika kwao pale wanapokuwa hawana weledi wa kuwatibu wagonjwa hao, rufaa zao inatakiwa ziende kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyo karibu na maeneo yao.
Wanawajibu wa kuboresha mawasiliano na wataalamu wa vituo vya serikali vilivyopo kwenye maeneo hayo.
Pamoja na hayo pia hawaruhusiwi kufanya matibabu kwa baadhi ya magonjwa ambayo hawana uwezo wa kuyatibu kama:-
Kila Mganga wa tiba asili anawajibu wa kutunza mazingira na kuboresha pale anapotelea huduma.
Tunduma-Momba
Postal Address: S.L.P 273 Tunduma Momba
Telephone: 0252957476
Mobile: 025 295 7476
Email: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc