Afisa lishe wa Mkoa wa Songwe Ndugu. Gerald Mlewa leo tarehe 09.11.2022 amefika halmashauri ya Wilaya ya Momba kutoa mafunzo ya badgeti ya namna ya kutengeneza bajeti ya lishe na namna ya kuitekeleza kimkakati katika Halmashauri yetu ili kuleta tija na kuweza kujikwamua katika swala la lishe duni na udumavu.
Aidha amewataka wakuu wote wa vitengo kuchukulia uzito swala la Lishe na kutenga bajeti mahususi kwajili ya kutekeleza shughuli zote za lishe zilizo pangwa kwa mwaka wa fedha husika na kuwa na mpango mkakati wa namna ya kufikia matarajio yaliyo wekwa.
Alihitimisha kwa kumsihi Afisa lishe wa wilaya kusimamia na kuhakikisha siku ya lishe inafanyika kw kila kijiji na pia kuhakikisha anazitembelea na kuanzisha clabu za lishe katika kila shule .
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc