KIKAO CHA TATHMINI YA MKATABA WA LISHE KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU YA MWAKA WA FEDHA 2023/2024
Picha na Matukio wakati wa kikao cha tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba leo tarehe 20 Mei 2024.
Kikao hicho ambacho kimewahusisha Watendaji wa Kata zote 14 za Halmashauri ya Wilaya ya Momba, kimefanyika kwa lengo la kupitia Kadi Alama kwa kuangalia hali ya utoaji wa chakula shuleni kwa wanafunzi.
Aidha, kikao hicho kimejadili utekelezaji wa taarifa za lishe kubandikwa kwenye mbao za matangazo katika ofisi zote za mitaa na kata.
Pia, pamoja na mambo mengine kikao hicho cha tathmini ya Mkataba wa lishe kimepitia na kujadili hali ya uibuaji wa watoto wenye utapiamlo.
Aidha, kikao hicho kimepokea taarifa ya maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe kwenye Mitaa kwa kipindi cha robo ya tatu ya Mwaka wa fedha 2023/2024.
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc