Friday 20th, September 2024
@CHITETE-SONGWE
TUMEFURAHISHWA SANA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO HALMASHAURI YA WILAYA YA MOMBA. - Mwenyekiti Mwampashi
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe imewapongeza viongozi wa Serikali ya Wilaya ya Momba pamoja na Halmashauri ya Momba kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa leo Terehe 23 Januari, 2023 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndugu Radwel Mwampashi wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wiaya ya Momba.
Akitoa majumuisho ya ziara hiyo, Ndugu Mwampashi amesema kuwa miradi waliyoitembelea katika ziara ya sasa imewafurahisha zaidi na ameziomba Halmashauri nyingine ziende Momba kujifunza Namna bora ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
"Miradi ya safari hii imetufurahisha sana kwa kweli kwa niaba ya kamati ya siasa nawapa 'Big up sana'. Nawapongeza sana. Hakuna mradi ambao umekuwa na kasoro na siku zote Halmashauri ya Wilaya ya Momba imekuwa roal modal ya Mkoa wa Songwe. Hongereni sana" amesema Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Songwe na kuongeza;
"Mimi kwa niaba ya kamati niwapongeze sana viongozi wa Halmashauriya Wilaya ya Momba. Kazi mnayoifanya ni nzuri lakini pia mambo yanayofanyika mazuri kama haya ni juhudi za
Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye usiku na mchana halali usingizi kuhakikisha wananchi wanapata huduma"
Katika ziara hiyo ambayo kamati ya Siasa iliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mheshimiwa Dkt. Francis Michael, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bi. Happiness Seneda, wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa Machinjio ya kisasa katika soko la kimataifa kakozi awamu ya tatu ( 2,000,000,000.00), Ujenzi wa Vyumba 3 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo shule ya msingi Nakawale (81,000,000.00) na Ujenzi wa Maternity complex Hospitali ya Wilaya ya Momba.
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc