Wilaya ya Momba, ni miongoni mwa wilaya mpya, ilianzishwa rasmi mwaka 2012 na Serikali kwa mujibu wa kifungu cha tano (5) sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), sura namba 287 R.E 2012 na pamoja na sheria nyinginezo zinazohusika na uanzishwaji wa Wilaya ni pamoja na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya uanzishwaji wa mikoa na Wilaya sura namba 397 ya mwaka 2012, baada ya kugawanya kwa Wilaya ya Mbozi kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa Wilaya ya Momba, kufuatia tangazo la Serikali (GN ) Namba 73 la mwaka 2012 wilaya ya Momba ilitangazwa kuanzishwa rasmi pamoja na wilaya nyingine 18, hati rasmi ya uanzishwaji wa wilaya ya Momba na kuanza kutumika ilitolewa tarehe 23/12/2012.
Wilaya ya Momba inaundwa na halmashauri mbili , halmashauri ya Wilaya ya Momba na halmashauri ya Mji wa Tunduma, ambazo kwa pamoja zina tarafa 4, halmashauri ya wilaya ya Momba ikiwa na tarafa 3 na jimbo moja la uchaguzi na halmashauri ya Wilaya ya mji wa Tunduma ikiwa na tarafa 1 na jimbo moja la uchaguzi.
Wilaya ya Momba inapatikana Magharibi mwa Mkoa mpya wa Songwe, kati ya Latitudo 80 10” Kusini na 90 15”kusini mwa mstari wa Equator, Longitudo 320 5’Mashariki na 320 45” Mashariki mwa mstari wa Greenwich ya Meridian. Wilaya inapakana na Mkoa wa Rukwa na Nchi ya Zambia upande wa Magharibi, Upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Mbozi, Upande wa Kaskazini inapatikana na Wilaya ya Chunya, na kusini inapakana na Wilaya ya Ileje.
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc