Shughuli kuu ya kiuchumi kwa wakazi wa wilaya ya Momba ni Kilimo ambapo asilimia 80 ya wakazi hutegemea kilimo. Katika kilimo, fursa zilizopo katika mazao ya kilimo ni kama ifuatayo:-
Pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Momba kuwa na fursa nyingi kama ilivyoainishwa hapo juu, mazao ya Mpunga na Mtama yanaweza kuleta matokeo ya haraka kwa wananchi katika kuinua kipato chao na kuwa malighafi za uhakika katika kuanzisha viwanda vya kusindika mazao hayo. Hii itasaidia kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao hayo.
2.1.2 KWA NINI MPUNGA NA MTAMA
Mpunga
Mtama
2.1.3 JITIHADA ZILIZOFANYIKA
Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi pamoja na Umwagiliaji kanda ya Mbeya imejenga Skimu ya umwagiliaji ya Naming’ongo kwa ajili ya zao la mpunga. Kwa sasa eneo lenye miundombinu ya umwagiliaji ni hekta 1,500 zinazolimwa. Uzalishaji Kwa mwaka unatarajiwa kufikia tija ya tani 6 kwa Hekta, hivyo kutoa jumla ya tani 9,000 kwa Hekta 1,500.
Pia halmashauri kupitia mradi wa SAGCOT-CTF unaotekelezwa na Kampuni ya Mtenda imetoa mafunzo kwa wakulima 41 kuhusu kilimo cha biashara na elimu ya ujasriamali. Mradi tayari umeajiri Afisa Kilimo Mmoja ambaye atashughulikia utekelezaji wa mradi huo katika wilaya ya Momba eneo la Naming’ongo.
Halmashauri kupitia mradi wa MIVARF imewezesha uanzishwaji wa vikundi 76 katika kata nne za Ivuna, Mkomba, Chilulumo na Mkulwe na chama kimoja cha ushirika katika kata ya Kamsamba. Vikundi hivi vina jumla ya wakulima 1,835 ikiwemo wanawake 1,004 na wananume 831 wanaojishughulisha na kilimo cha mpunga. Vikundi hivi vinalima jumla ya hekta 1,944 ambazo huzalisha tani 4,747.68 kwa mwaka.
Halmashauri kuanzia mwaka 2015 imehamasisha wananchi kulima zao la mtama kwa kuwa zao hili lina soko la uhakika na Uhakika wa kuvuna upo kwa vile linavumilia ukame.
Katika mavuno ya msimu wa 2015/16 halmashauri iliwaunganisha wakulima na kampuni ya Rapha group ambayo ilinunua tani tani 1,200 za mtama katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba.
Aidha Halmashauri imefanya mazungumzo ya kuwaunganisha wakulima wa zao la mtama kwenye kilimo cha mkataba na kampuni ya OBO investment ambayo ipo tayari kununua tani 15,000 za mtama.
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc