TUNAPASWA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA BIDII.
Ikiwa ni kilele cha ziara ya siku tatu(3) ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba amewataka Watumishi wa Umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba kutambua wajibu wao kwa jamii na kufanya kazi kwa bidii ambapo kwa kufanya hivyo kero nyingi za wananchi zitatatuliwa.
Bi. Seneda ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Momba katika Shule ya Sekondari chikanamlilo mara baada ya kumaliza ziara yake leo hii Novemba 09, 2023 aliyoifanya huku akiwa ameambatana na baadhi ya Wajumbe wa Timu ya Sekretarieti ya Mkoa wa Songwe.
Aidha Bi. Seneda alisema,
"Watumishi wenzangu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetupa wajibu mkubwa wa kuwatumikia Wananchi na kutatua kero zao na si vinginevyo, hivyo, wajibu huu tuubebe kwa thamani kubwa na wakati huo huo maslahi na stahiki zenu zinashughulikiwa."
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc