Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Momba limepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 huku ikitegemea kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 2 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani.
Akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka 2023/2024 mbele ya Baraza la Madiwani Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Momba Ndg. Alex Batueli amebainisha kuwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Momba inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 26 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani serikali kuu na wahisani.
Katika rasimu ya bajeti hii imeshauriwa kila mradi uliombanga kupelekewa Fedha za Miradi wajiandae mapema ikiwa ni pamoja na kuandaa vitendea kazi kama tofari, mchanga na kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika kuchangia nguvukazi kwenye miradi ya maendeleo
Aidha baadhi ya madiwani wamesema kuwa bajeti italeta tija katika maendeleo kwani imejaribu kugusa katika kila maeneo kama ya Elimu, Afya na kilimo.
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc