KIKAO KAZI CHA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA KATA 14 ZA HALMASHAURI ZA WILAYA YA MOMBA.
Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Momba Bi. Rehema Muhunzi leo Tarehe 08 Mei 2024 ameongoza kikao kazi cha Maafisa maendeleo ya Jamii kutoka kata zote 14 pamoja na Maafisa wengine wa ngazi ya wilaya ambapo katika kikao hicho wamejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwasilishwaji wa Taarifa za utekelezaji wa kazi mbalimbali katika jamii,
Aidha katika kikao kazi hicho Bi, Rehema ameweza kuendesha mafunzo ya matumizi sahihi ya Mfumo wa kujihudumia kwa watumishi wa Umma ESS (PEPMIS).
Pia kupitia kikao kazi hicho Mkuu wa divisheni hiyo Bi. Rehema Muhunzi ametoa maelekezo mbalimbali ikiwemo Kutoa Elimu kwa vikundi na kutengeneza katiba zao, kufanya Utembeleaji wa miradi ya ujenzi wa vyoo pamoja na kituo cha Afya na kutoa vyeti vya watoto vya kuzaliwa,
na Utekelezaji na kuwakumbusha Jamii katika kukamilisha miradi.
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc