Serikali ya Halmashauri ya wilaya ya Momba imeanza mkakati wa kutoa elimu na kuimiza kwa kila mwananchi mwenye umri kuanzia miaka 18 kuchangamkia fursa ya kilimo cha ufuta na korosho ambacho kimeonekana kufanya vizuri na kwa tija kwa wakulima wa Momba.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Momba, Mhe. Methew Chikoti amesema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi na kusikiliza kero za wananchi akiambatana na waheshimiwa madiwani wa kamati ya fedha, mipango na uongozi.
Mhe. Methew Chikoti amesema Halmashauri imejipanga na imeisha andaa mbegu bora ya ufuta na korosho kwa ajili ya kuwagawia wananchi kwa utaratibu mzuri ambao umepangwa na watalamu.
"Tunataka kuona kila kaya ndani ya Momba inalima ekari moja ya ufuta au zaidi na kwa zao la korosho lengo letu ni kuona kila kaya inaandaa na kulima nusu eka ya korosho ili wakulima wetu wapate fedha kupitia mazao aya na kuondokana kutegemea kilimo cha mpunga na mahindi" Mhe. Methew Chikoti.
Pia, Mhe. Methew Chikoti ametoa onyo na tahadhari kwa vijana ambao watashindwa kulima korosho na ufuta watakamatwa na Serikali za vijiji vyao na watapewa adhabu ya kwenda kulima kwenye mashamba ya wenzao waliolima ufuta na korosho bila kulipwa chochote.
Lengo letu ni kuona kila moja analima na kupata fedha kwa ajili ya kukuza uchumi wa familia yake pamoja na Halmashauri ya Momba.
Afisa Kilimo Halmashauri ya Momba, Mathew Kyando amesema kila kata inayolima korosho na ufuta tayari ina watalamu wa kilimo ambao watawashauri kitalamu wakulima.
Mathew Kyando amesema mbegu za korosho zitatolewa bure kwa kila mkukima ili aweze kulima nusu Ekari ambayo ni sawa na miti 13 ya korosho pamoja na viwatilifu vyake vya korosho na kwa wakulima wa ufuta watapata mbegu bora kwa nusu bei.
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc