WAGANGA WA TIBA ASILI MKASTAWISHE JAMII NA SIO KUTENGANISHA JAMII
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba Ndg. Alex Batweli
Leo tarehe 07 mei 2024 katika Hafla ya kukabidhi vyeti kwa Waganga wa Tiba Asili amewataka waganga hao kuwa sehemu ya Kustawisha Jamii na sio Kwenda kutenganisha jamii katika maeneo yao.
Aidha kupitia Hafla hiyo Batweli amewasisitiza Wataalamu wa Tiba Asili kutoa taarifa zao za kitabibu na pia kutoa rufaa ya wagonjwa wanaofika kwao pale wanapokuwa hawana weledi wa kuwatibu wagonjwa hao, rufaa zao inatakiwa ziende kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyo karibu na maeneo yao.
“Mnawajibu wa kuboresha mawasiliano na wataalamu wa vituo vya serikali vilivyopo kwenye maeneo yenu” Alex Batweli.
Tunduma-Momba
Anwani: S.L.P 273 Tunduma Momba
Namba ya Simu: 0252957476
Simu: 025 295 7476
Barua Pepe: ded@mombadc.go.tz
Haki zote zimeifadhiwa ©2018 Momba dc